1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Umeme wakatika kote nchini Venezuela

31 Agosti 2024

Umeme ulikatika kote nchini Venezuela ikiwa ni pamoja na mji mkuu Caracas kuanzia jana alfajiri.

Giza likitanda katika mji mkuu wa Venezuela Caracas baada ya kukatika kwa Umeme
Giza likitanda katika mji mkuu wa Venezuela Caracas baada ya kukatika kwa UmemePicha: Ariana Cubillos/AP Photo/picture alliance

Kukatika kwa umeme kumeathiri pakubwa shughuli za kijamii katika taifa ambalo linakabiliwa na mzozo wa kisiasa tangu uchaguzi wa Julai 28.

Waziri wa Mawasiliano Freddy Nanez amelielezea tukio hilo kuwa ni hujuma, uhalifu na jaribio la mapinduzi ya kijeshi, mwezi mmoja baada ya uchaguzi wenye utata uliompa  ushindi rais Nicolas Maduro.

Umeme ulikuwa ukirejea na kukatika tena katika baadhi ya maeneo ya Caracas na katika majimbo ya kusini-magharibi ya Tachira na Merida. Serikali hata hivyo imeahidi kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo.

Mara kadhaa mamlaka nchini humo zimekuwa zikisema kuwa vitendo vya hujuma huendeshwa na Marekani kwa ushirikiano na upinzani ili kuipindua serikali.