1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiGuinea-Bissau

Umeme warejeshwa Bissau baada ya serikali kulipa deni

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2023

Kampuni ya Kituruki ya Karpowership, imerejesha umeme katika mji mkuu wa Guinea-Bissau baada ya serikali kuanza tena kulipa deni la kampuni hiyo.

Bissau
Guinea-BissauPicha: Iancuba Dansó/DW

Kampuni ya Kituruki ya Karpowership, imerejesha umeme katika mji mkuu wa Guinea-Bissau baada ya serikali kuanza tena kulipa deni la kampuni hiyo. Waziri wa uchumi wa Guinea-Bissau Suleimane Seidi aliwaambia waandishi wa habari jana Jumatano kwamba serikali imeweza kulipa kiasi cha dola milioni 6 kati ya 15 za malimbikizo ambazo inadaiwa.Kampuni hiyo ya Kituruki ilizima umeme katika taifa hilo la Afrika Magharibi kutokana na deni la dola milioni 17.

Guinea Bisau imekuwa ikitegemea kampuni hiyo ya umeme ya Uturuki kukidhi asilimia 100 ya mahitaji yake ya umeme tangu makubaliano yao ya mwaka 2019. Mnamo Septemba, kampuni hiyo ilizima usambazaji umeme katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown kutokana na deni la takriban dola milioni 40.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW