1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMMA UAMSHWE KUPINGA VITA:

18 Januari 2004
MUMBAI: Wanaharakati mashuhuri wa kimataifa wanaopigania amani duniani,hii leo wametoa muito kuwa umma katika kila pembe ya dunia unapaswa kuamshwa kupinga vita.Chandra Muzzafar wa Malaysia akizungumza mjini Mumbai katika Kongomano la Kijamii Duniani-"World Social Forum" amelaani utumizi wa nguvu wa Marekani dhidi ya nchi zingine.Akasema lazima Marekani na washirika wake washinikizwe ili kuwazuia kwenda vitani.Na Abdul Amir Rebaky kutoka Iraq amesema wimbi kuu hivi sasa katika ulimwengu wa Kiarabu ni kupigania haki bila ya kutumia nguvu na kwamba ile picha inayotolewa kuwa wao ni watu wenye ghasia na fujo si sawa.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW