1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika unasaka njia za kurejesha nidhamu Mauritania

9 Agosti 2005

Nouakchott:

Ujumbe wa Umoja wa Afrika umewasili Mauritania kwa lengo la kusaka njia za kuheshimiwa katiba na kurejeshwa nidhamu nchini humo.Duru za kuaminika kutoka mji mkuu wa Mauritania Nouakchott zinasema ujumbe huo utakua na mazungumzo hii leo pamoja na rais wa baraza la kijeshi kwaajili ya haki na demokrasia,kanali Ely Ould Mohammed Vall.Haijulikani lakini kwa muda gani ujumbe huo utasalia nchini Mauritania.Ujumbe huo unaoongozwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Nigeria Oluyemi Adeniji,unawajumuisha pia waziri wa usalama wa Afrika Kusini na dhamana mmoja wa kamisheni ya Umoja wa Afrika.Marekani imesema jana inaunga mjkono juhudi za Umoja wa Afrika za kurejesha nidhamu nchini Mauritania.Haishikilii tena lakini arejeshwe madarakani rais aliyepinduliwa Maaouiya Ould Taya.Mapinduzi ya amani ya agosti tatu iliyopita yanasemekena yanaungwa mkono na wananchi wengi wa Mauritania.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW