1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika unasita kwa muda kutuma wanajeshi Darfour

3 Septemba 2005

Umoja wa Afrika umesitisha hadi september 19,mpango wa kutuma wanajeshi katika eneo la mzozo la Darfour-magharibi ya Sudan.Taarifa ya Umoja wa Afrika iliyochapishwa mjini Addis Ababa inasema uamuzi huo umepitishwa kutokana na ukosefu wa mafuta na hali mbaya ya hewa .Mpango huo huenda ukaanza upya september 19 na kuendelea hadi october 22 ijayo-taarifa hiyo imesema.Tume ya Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfour inajumuisha wanajeshi elfu sita kwa sasa.Umoja wa Afrika unapanga kuzidisha idadi yao hadi wanajeshi 7700 hadi october 22 ijayo.Vikosi vya amani vya umoja wa Afrika vinasimamia makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa april mwaka jana -makubaliano ambayo mara kwa mara yamekuwa yakiendewa kinyume na pande zinazohusika na mzozo nwa Darfour.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW