Umoja wa Afrika wachanga fedha kusaidia wahanga wa ukame
26 Agosti 2011Matangazo
Mkutano huo wa kilele umehudhuriwa na viongozi wanne tu wa taifa na serikali, ikiwa ni wachache kuliko ilivyotarajiwa. Benki ya Maendeleo ya Afrika imeahidi msaada wa dola mlioni 300. Mkurugenzi wa shirika la misaada la Oxfam barani Afrika, Irungu Houghton amesikitika kuwa serikali za Afrika hazukushughulikia vya kutosha tatizo hilo.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, bado kunahitajiwa dola bilioni 1.1 ili kuweza kuzuia madhara makubwa zaidi kutokana na ukame mbaya kabisa kushuhudiwa tangu miongo kadhaa katika Pembe ya Afrika. Zaidi ya watu milioni 12 wanakabiliwa na njaa nchini Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Kenya na Uganda.