Umoja wa Afrika waitoa Niger katika shughuli zake zote
22 Agosti 2023Matangazo
Aidha, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, limepitia maamuzi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS ya kupeleka wanajeshi nchini Niger. Limeitaka halmashauri ya muungano wa Afrika kutathmini athari za kiuchumi, kijamii na kiusalama za uingiliaji kati kijeshi.
Jumuiya ya ECOWAS ilisema kuwa iko tayari kuwatuma wanajeshi nchini Niger, endapo juhudi za kidiplomasia zitashindikana.
ECOWAS yasema LA, kwa pendekezo la utawala wa kijeshi Niger
Umoja wa Afrika umetoa wito kwa wanachama wake wote na jumuiya ya kimataifa kujizuia na hatua yoyote inayoweza kuhalalisha utawala wa kijeshi wa Niger.
Lakini wakati huohuo umekataa uingiliaji kati wa nchi yoyote nje ya afrika.