Umoja wa Afrika wakutana kuzungumzia Kongo
27 Desemba 2012Matangazo
Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika mjini Addis-Ababa, Ethiopia, ukiwa unahudhuriwa na viongozi wa Kanda ya Maziwa Makuu, maafisa wa Umoja wa Ulaya na wawakilishi kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ghasia zilizuka eneo hilo la mashariki mwa Kongo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma.
Mapema mwezi huu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ilisema iko tayari kupeleka kikosi cha kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Josephat Charo