1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU yamtaka Rais Sall kuitisha uchaguzi wa rais Senegal

5 Februari 2024

Umoja wa Afrika umeitaka Senegal iitishe uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo. Tamko la Umoja wa Afrika limetolewa siku chache baada ya rais wa Senegal Macky Sall kutangaza kuchelewesha kwa muda usiojulikana.

Senegal I  Macky Sall
Rais wa Senegal Macky SallPicha: Amr Alfiky/File Photo/REUTERS

Umoja wa Afrika umeitaka Senegal iitishe uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo. Tamko la Umoja wa Afrika limetolewa siku chache baada ya rais wa Senegal Macky Sall kutangaza kuchelewesha kwa muda usiojulikana, uchaguzi huo uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu.

Senegal haijawahi kuchelewesha uchaguzi wa rais na hatua ya rais Macky Sall aliyoitangaza Jumamosi imeitumbukiza nchi hiyo katika hali ya wasiwasi huku baadhi ya wapinzani na mashirika ya kiraia wakiita ni mapinduzi ya katiba.

Jana usiku mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Moussa Faki Mahamat alitoa tamko akisema Senegal inapaswa kuitisha uchaguzi haraka iwezekanavyo utakaofanyika kwa njia ya uwazi,na amani.

Bunge linatarajiwa leo Jumatatu kujadili pendekezo juu ya kuitisha uchaguzi huo tarehe 25 mwezi Agosti na kumuacha rais Macky Sall kuendelea kuwa madarakani hadi mrithi wake atakapopatikana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW