1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika waonesha wasiwasi maandamano Kenya

28 Machi 2023

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amesema ana wasiwasi mkubwa baada ya maandamano ya kuipinga serikali nchini Kenya kugeuka kuwa machafuko na ametowa mwito wa utulivu.

Kenia | Ausschreitungen und Proteste in Nairobi und Kisumi
Picha: John Muchucha/REUTERS

Kupitia taarifa yake mwenyekiti huyo wa Tume ya Umoja wa Afrika amewataka wadau wote nchini humo kuwa na utulivu na kuingia kwenye mazungumzo kushughulikia tafauti zao kwa maslahi ya mshikamano na maridhiano ya kitaifa. 

Soma zaidi: Kenya yagawika ikielekea uchaguzi mpya wa Rais Okt 26

Jana (Machi 27) polisi walifyetua mabomu ya kutowa machozi jijini Nairobi na mji wa magharibi mwa Kenya wa Kisumu ambako ni ngome ya kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, kuwatawanya waandamanaji.

Watu kadhaa waliuwawa na mali kuharibiwa nchini humo. Miongoni mwa mali zilizoharibiwa ni shamba la rais wa zamani, Uhuru Kenyatta, na kampuni ya Odinga.