1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanachama AU wapinga Macky Sall kugombea ukatibu mkuu UN

28 Machi 2026

Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) zimekataa kumuunga mkono Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kuchukua nafasi ya Antonio Guterres.

Macky Sall amekosa kuungwa mkono na nchi za AU kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa UN
Rais wa zamani wa Senegal Macky SallPicha: John Thys/AFP

Kulingana na taarifa, jumla ya nchi 20 wanachama wa AU, ambazo hazikutajwa zimepinga ugombea wa Macky Sall, aliyeiongoza Senegal kuanzia 2012 hadi 2024 na ambaye pia hakuungwa mkono hata na nchi yake.

Shutuma za usimamizi mbaya wa nchi dhidi ya Sall enzi za utawala wake

Ugombea wa Sall uliwasilishwa na Burundi, inayoshikilia urais wa kupokezana wa Umoja wa Afrika, lakini viongozi wa sasa ya Senegal ikiwa ni pamoja na Rais Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu Ousmane Sonko, wanawashutumu viongozi wa zamani, hasa Macky Sall, kwa usimamizi mbaya wa nchi na kuyazima kwa nguvu maandamano ya kisiasa yaliyosababisha vifo vingi vya raia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW