1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Umoja wa Afrika wasimamisha uanachama wa Gabon

1 Septemba 2023

Umoja wa Afrika, umesimamisha uanachama wa Gabon baada ya mapinduzi ya kijeshi katika taifa hilo la Afrika ya Kati. Umoja huo umesimamisha ushiriki wa Gabon katika shughuli zake na taasisi zake zote mara moja

Mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia mnamo Februari 18, 2023
Mkutano wa Umoja wa Afrika nchini EthiopiaPicha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Siku ya Alhamisi (31.08.2023) baraza la amani na usalama la Umoja huo, lilisema kuwa linalaani vikali mapinduzi hayo yaliomuondoa madarakani rais Ali Bongo. Wiki chache zilizopita, Umoja huo wa Afrika pia ulisimamisha uanachama wa Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Julai.

Soma pia:Viongozi wa Afrika kujibu hatua ya mapinduzi ya kijeshi Gabon

Uanachama wa Burkina Faso, Mali, Guinea na Sudan katika Umoja huo pia umesimamishwa tangu mapinduzi ya kijeshi katika mataifa hayo.

Umoja wa Ulaya wapinga mapinduzi ya kijeshi Gabon

Katika hatua nyingine, mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amesema kuwa Umoja huo unapinga kutwaliwa kwa nguvu kwa mamlaka nchini Gabon. Katika taarifa, Borrell amesema kuwa changamoto zinazoikabili Gabon lazima zitatuliwe kulingana na kanuni za sheria, utaratibu wa kikatiba na demokrasia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW