1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU: Yataka kusitishwa vita kati ya Israel na Ukanda wa Gaza

9 Oktoba 2023

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ametoa wito wa kusitishwa mzozo kati ya Israel na kundi la wapiganaji wa Palestina, Hamas, ambao umesababisha vifo vya mamia ya watu kutoka pande zote mbili.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mahamat Moussa Faki
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mahamat Moussa FakiPicha: John Thys/AFP

 Mkuu huyo wa Umoja wa Afrika amezitaka pande zote mbili kurejea kwenye meza ya mazungumzo bila masharti hatua ambayo itatekeleza kanuni ya mataifa mawili ya kuishi bega kwa bega.

Mwenyekiti huyo wa Tume ya Umoja wa Afrika pia ameoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, na hasa mataifa makubwa yenye nguvu duniani, kubeba jukumu la kuweka amani na kulinda haki za watu wa Israel na Wapalestina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW