Umoja wa Afrika watowa wito wa kusitishwa vita nchini DRC
10 Februari 2026
Rais wa Angola ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, pamoja na viongozi wengine wametowa mwito wa kusitishwa vita mashariki mwa Kongo, baada ya kufanyika mazungumzo na rais Felix Tschisekedi.
Jana Jumatatu mjini Luanda, ulifanyika mkutano uliowashirikisha viongozi mbali mbali na kutolewa mwito wa vita kusitishwa.
Katika taarifa yake Joao Lourenco alitowa mwito huo akizitaka pande zote zinaziohusika na mgogoro huo wa Mashariki mwa Kongo kutangaza utekelezaji wa usitishaji vita katika muda uliokubaliwa chini ya makubaliano yaliyofikiwa Doha mwezi Oktoba mwaka 2025.Rwanda yajiunga na ukosoaji wa utawala mbadala wa M23
Tamko hilo la Lourenzo lilisainiwa na Tshisekedi pamoja na kiongozi wa Togo Faure Gnassingbe na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ambao waliteuliwa kwa pamoja kama wasuluhishi na wasimamizi waUmoja wa Afrikawa mchakato wa amani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Viongozi hayo pia walitangaza kuunga mkono makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani wakisema Angola itawajibika kuanzisha mashauriano pamoja na pande zote zinazohusika upande wa Kongo.
Qatar kwa miezi kadhaa imekuwa ikiendesha juhudi za usuluhishi kati ya serikali ya Kongo na M23 na ahadi ya kuzingatia makubaliano ya kusitisha vita ilisainiwa mwezi Julai.
Wakati juhudi za kutafuta amani zikiendelea ndani ya Kongo kwenyewe ripoti za jeshi zilizotolewa Jana zimesema waasi wanaoungwa mkono na kundi linalojiita dola la Kiisalamu walishambulia mwihsoni mwa juma katika kijiji kimoja mashariki mwa nchi hiyo na kuuwa takriban watu 20.Mataifa ya Maziwa Makuu kuhusishwa katika juhudi za kuutatua mgogoro wa DRC
Shambulio hilo lililofanywa na waasi wa Allied Democratic Forces ADF lilitokea Jumamosi kwenye kijiji cha Mambimbi-Isigo katika eneo la Lubero mkoani Kivu Kaskazini, kwa mujibu wa ripoti ya kiongozi wa jeshi kwenye eneo hilo kanali Alain Kiwewa Mitela.
Hata hivyo kundi la ADF halikutowa tamko lolote kwa haraka japo imeelezwa kwamba shambulio walilolifanya lilisababisha wakaazi chungunzima kuachwa bila makaazi na kuongeza makali ya hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa.
Wanaharakati wa mashirika ya kiraia kwenye eneo hilo waasi hao walianza kuvamia mashamba kadhaa kabla ya kuwageukia raia na kuwashambulia kwa visu na kuwafyetulia risasi.
Mkuu wa mashirika ya kiraia katika eneo la Bapere Kinos Kitwa amekosoa kikosi kidogo cha jeshi kilichoko kwenye eneo hilo huku akisema kuna raia wengi ambao hawajulikani waliko.Mgogoro Kongo Mashariki wachochea hofu ya vita vya kanda
Kundi la ADF ambalo lilijitangaza kuliunga mkono kundi linalojiita dola la Kiislamu mnamo mwaka 2019 linaendesha hujuma zake kwenye eneo la mpaka kati ya Uganda na mara nyingi likiwalenga raia.
Takriban raia 62 wameuwawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu na kundi hilo la ADF katika maeneo ya Beni na Lubero.