Umoja wa Afrika yaisimamisha uanachama Cote d'Ivoire.
10 Desemba 2010Matangazo
Afisa mmoja wa Umoja huo, amesema Cote d'Ivoire itasimamishwa uanachama mpaka pale kiongozi wa upinzani, Alassane Ouattara atakaposhika madaraka kutoka kwa mpinzani wake rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo.
Mpaka sasa bwana Gbagbo bado anakataa kuachia madaraka, licha ya matokeo rasmi ya uchaguzi na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kusema kwamba mpinzani wake ameshinda uchaguzi.
Viongozi wote hao, Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara, kila mmoja anadai kushinda uchaguzi huo, hali ambayo jumuia ya kimataifa imebidi kuingilia kati.