1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Syria yawazika watu waliouawa katika shambulizi

6 Oktoba 2023

Syria Ijumaa hii imefanya mazishi ya watu kadhaa waliouawa kwenye shambulio la ndege isiyo na rubani jana Alhamisi katika sherehe za mahafali.

Vikosi vya usalama vikijaribu kuondoa vifusi katika jengo lililoshambuliwa katika eneo la Areha nchini Syria, Oktoba 5, 2023
Vikosi vya usalama vikijaribu kuondoa vifusi katika jengo lililoshambuliwa katika eneo la Areha nchini Syria, Oktoba 5, 2023Picha: Ghaith Alsayed/AP/picture alliance

Shambulio hilo baya zaidi katika miaka 12 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe lilifanyika kwenye sherehe ya mahafali katika chuo cha kijeshi kwenye mkoa wa Homs.

Watu 112 waliuawa jana katika shambulio hilo na wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa.

Jeshi la Syria limeahidi kujibu vikali shambulio hilo na kusema limefanywa na makundi ya kigaidi kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizojazwa mabomu.

Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na tukio hilo.

Geir Pedersen, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria amesema katika taarifa yake kuwa matukio hayo ya kutisha ni ukumbusho kuhusu umuhimu wa kukomeshwa mara moja ghasia, kuelekea usitishaji vita nchi nzima na kuwepo mwelekeo wa ushirikiano katika kukabiliana na makundi ya kigaidi yaliyoorodheshwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW