1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefungua njia ...

16 Januari 2004
kwa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kutuma kikosi cha kwanza cha jeshi lake jipya hadi mjini Kisangani, mashariki mjwa Kongo. Azimio lililokubaliwa kwa kauli moja na baraza hilo la mataifa 15, limeidhinisha kutumwa askari jeshi wa kwanza 2 400 hadi Kisangani, ambao umekuwa ukidhibitiwa na waasi ambao walikuwa wakipigana na serikali iliopita mjini Kinshasa. Kikosi hiki, kikiwa cha kwanza cha mchanganyiko baina ya waasi na wanajeshi wa serikali, ni hatua ya kwanza ya kuimarisha jeshi jipya la kitaifa.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW