1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Kuanza kuwaondoa askari wa kulinda amani kutoka DR Kongo

19 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukubaliana na matakwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na hivyo kutangaza mpango wa kuwaondoa askari wa kulinda amani huko hatua kwa hatua kuanzia baadaye mwezi huu.

Demokratische Republik Kongo | MONUSCO Mission | Goma
Picha: Olivia Acland/REUTERS

Uamuzi huo umefikiwa licha ya Umoja wa Mataifa kuwa na wasiwasi kuhusu ghasia katika eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati huu ikijiandaa uchaguzi wa rais, wabunge na wa serikali za mitaa utakaofanyika hapo kesho, Jumatano.

Wanajeshi wa Jumuiya ya EAC kuondoka Kongo ndani ya siku 30

Uchaguzi huo unafanyika sambamba na kumalizika kwa muda wa majukumu ya kila mwaka ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, nchini humo (MONUSCO). Kuanzia mwezi Mei mwaka ujao wa 2024, MONUSCO itakuwepo Kivu Kaskazini na Ituri.

Na kuanzia Julai 1, wahudumu wake 2,350 watapunguzwa.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW