1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

UN kuchunguza uuzwaji wa chakula cha msaada Ethiopia

11 Aprili 2023

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linachunguza wizi wa chakula cha msaada kupitia operesheni za kiutu nchini Ethiopia, hii ikiwa ni kulingana na barua ambayo shirika la habari la AP iliipata.

Äthiopien Tigray Konflikt Symbolbild
Picha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Barua hiyo iliyoandikwa na mkurugenzi wa WFP nchini humo Claude Jibidar na kutumwa kwa washirika wake kwenye taifa hilo, ambako watu milioni 20 wanategemea misaada kutokana na ukame mkali na mzozo wa ndani.

Barua hiyo ya Aprili 5, imeonya juu ya mauzo yanayotia wasiwasi ya chakula cha msaada na kutaka kuchukuliwa hatua ili kuzuia matumizi mabaya ya msaada nchini humo.

Jibidar amewatolea wito washirika wake kushirikishana taarifa zozote ama visa vya matumizi mabaya ya chakula hicho vinavyowasilishwa na wafanyakazi wao, watumiaji ama mamlaka ya maeneo husika, ingawa barua hiyo haikutaja kisa chochote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW