1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Umoja wa Mataifa kuzingatia rasimu ya vikwazo kwa Israel

3 Aprili 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea Haki za Binadamu litazingatia rasimu ya azimio linalotoa wito wa Israel kuwekewa vikwazo vya silaha, kutokana na kile linachosema ni "hatari ya kutokea kwa mauaji ya halaiki."

Gaza
Gari lililoharibiwa kwenye vita vya GazaPicha: Ali Jadallah/Anadolu/picture alliance

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea Haki za Binadamu siku ya Ijumaa litazingatia rasimu ya azimio linalotoa wito wa Israel kuwekewa vikwazo vya silaha, kutokana na kile linachosema ni "hatari ya kutokea kwa mauaji ya halaiki." 

Soma: Israel yasema shambulizi lililowauwa wafanyakazi wa misaada lilikuwa "kosa kubwa"

Rasimu hiyo imewasilishwa na Pakistan kwa niaba ya mataifa 55 kati ya 56 wanachama wa Umoja wa Mataifa katika Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu OIC.

Rasimu hiyo yenye kurasa nane inaitaka Israel iache kuyakalia maeneo ya Palestina na kufungua njia za misaada za kuingia Ukanda wa Gaza mara moja.

Iwapo rasimu hiyo itakubaliwa, hii itakuwa mara ya kwanza kabisa shirika hilo kuu la haki la Umoja wa Mataifa kuchukua msimamo kuhusiana na vita vya Israel dhidi ya Hamas. Papa asikitishwa na vifo vya wafanyakazi wa misaada Gaza

Hayo yakiarifiwa, Televisheni moja ya Misri imeripoti kuwa miili ya wafanyakazi sita wa kigeni waliouwawa katika msururu wa mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, imesafirishwa na kuingia nchini humo leo. Mashambulizi hayo ya Israel yameipelekea Israel kukosolewa kuhusiana na vitendo vyake katika vita hivyo vilivyodumu kwa kwa miezi sita sasa.