1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa: Mwito wa kuzisaidia nchi zisizojiweza

18 Novemba 2003

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, leo ameziomba nchi tajiri zichange Dollar billioni tatu mwaka ujao kwa lengo la kuokoa maisha ya watu millioni 45 katika nchi 21. Bw. Annan amesema kuwa raia hao wanakabiliwa na madhila mbalimbali, wamepoteza mali zao, nyumba zao, maisha yao yamevurugwa vibaya sana na vita, migogoro na mabalaa ya kimaumbile. Wengi wao ni watoto, wanawake na wazee. Katibu Mkuu amesema kuwa amani haiwezi kupatikana hata kidogo katika ulimwengu ambao unazidi kujaa neema na huku mamillioni ya watu wanaishi maisha ya dhiki. Fedha hizo zitatumiwa kununulia chakula, dawa na nyumba. Bw. Annan amemaliza kwa kusema kuwa mwito uliotolewa mwaka wa jana wa Dollar Billioni tano na nusu zilizopatikana zilikuwa asili mia 66. Nchi nyingi miongoni mwa hizo 21 ziko barani Afrika, hali kadhalika na Urussi, Chechenya, Jamhuri za zamani za Urussi na Korea ya Kaskazini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW