1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa na Angola kupeleka wanajeshi zaidi wa kuhifadhi amani katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ponda, Eric Kalume12 Novemba 2008

Jamii ya kimataifa sasa inaelekeza juhudi za kupeleka vikosi zaidi vya kuhifadhi amani katika katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambako mamia ya watu wameuawa na wengine wasiopungua 250,000 kuachwa bila makao.

Wakimbizi wanaotoroka mapigano nchini Kongo, wakiendelea kumiminika katika kambi za wakimbizi karibu na mji wa Goma.Picha: AP


Jamii ya kimataifa sasa inaelekeza juhudi za kupeleka vikosi zaidi vya kuhifadhi amani katika katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambako mamia ya watu wameuawa na wengine wasiopungua 250,000 kuachwa bila makao kufuatia uasi wa Wapiganaji wa Laurent Nkunda.


Huenda idadi ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa mataifa kinacho hifadhi amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikaongezwa hivi karibu, kufuatia hatua ya baraza hilo la Umoja wa Mataifa, kuondoa hali yake ya kusita sita kuhusu kupelekwa kwa wanajeshi zaidi katika eneo hilo la mashariki mwa Kongo.


Baada ya kukiarifu kikao cha baraza hilo kuhusu hali ilivyo katika, mwakilishi wa katibu mkuu Alain Le Roy ambaye amereja kutoka eneo hilo la mapigano, aliwaambia waandishi wa habari kuwa baraza hilo la usalama limependekeza nyongeza ya wanajeshi 3000 pamoja na polisi, ili kukiimarisha kiikosi cha wanajeshi 17.000 wa umoja wa mataifa walioko Congo hivi sasa.


Akaongeza kwamba wanachama wengi wamekubaliana na pendekezo hilo kwa kutumia utaratibu uliopendekezwa na Uafaransa , lakini bado hakuna uamuzi uliochukuliwa na baraza hilo, licha ya kwamba kumesisitizwa haja ya kuongezwa wanajeshi .


Pamoja na hayo waakilishi wa jumuiya ya haki za binaadamu wakizungumza na waandishi habari mjini Newyork, wameilitaka baraza hilo lichukua hatua za haraka.


Hata hivyo wakati hatua zikisubiriwa, Angola kwa upande wake imetangaza itatuma wanajeshi nchini Congo. Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Angola Georges Chicoty akitangaza hayo, hakutaja juu ya idadi wala majukumu ya wanajeshi hao.


Uamuzi wa Angola umekuja siku chache baada ya mkutano wa viongozi wa nchi za kusini mwa Afrika SADC, kuamua kutuma awanajeshi nchini Congo kuliimarisha jeshi la taifa.


Kwa upande mwengine, Katibu mkuu Ban Ki-moon amesema zaidi ya wakaazi 100.000 waliotawanyika wanahitaji msaada wa dharura nchini Congo, baada ya shughuli za misaada kukatwa kutokana na kuzuka mapigano mapya kati ya waasi na majeshi ya serikali.


Mashirika la kutetea haki za binadamu linasema kuwa hali ya wakimbizi katika eneo hilo la mashari, ni mbaya sana.










Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW