1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Katibu mkuu hana hatia kutokana na mkataba wa ukandarasi wa ukaguzi wa bidhaa nchini Iraq katika kampuni anayofanyia kazi mwanae Kojo.

29 Machi 2005

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan anatarajiwa kulaumiwa leo katika ripoti muhimu kwa kupuuzia uwezekano wa mgongano wa kimaslahi unaomhusu mwanae wa kiume Kojo, lakini hatashutumiwa kwa kufanya kosa hilo kwa ubinafsi.

Uchunguzi huru uliofanywa chini ya uongozi wa mwenyekiti wa zamani wa benki kuu ya Marekani , Bwana Paul Volcker, unatoa ripoti nyingine kuhusiana na mpango wa mauzo ya mafuta kwa ajili ya chakula wa umoja wa mataifa kwa Iraq, mara hii kumhusu katibu mkuu na mwanae Kojo, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Uswisi ya Cotecna. Kampuni hiyo ilipokea mkataba mkubwa wa umoja wa mataifa mwezi wa Januari 1999 ili kukagua bidhaa nchini Iraq.

Msemaji wa umoja wa mataifa Bwana Fred Eckhard amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisisitiza kila mara kuwa mkataba huo kwa Cotecna ulitolewa kwa mujibu wa taratibu za umoja wa huo , na kwamba katibu mkuu ataondolewa katika shutuma hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW