1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Madawa ya kulevywa yazalishwa zaidi, Afghanistan.

3 Septemba 2006

Umoja wa mataifa umesema kuwa kumekuwa na ongezeko la asilimia 60 katika kilimo cha mihadarati nchini Afghanistan mwaka huu.

Ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya mihadarati na uhalifu imesema kuwa zao kubwa kabisa linatoa tani 6,100 madawa hayo, ambayo yanauwezo wa kuzalisha tani 610 za madawa ya kulevywa.

Hii itakuwa ni asilimia 92 ya uoatikanaji wa madawa ya kulevywa duniani.

Mkuu wa ofisi hiyo, Mario Costa, amemtaka rais wa Afghanistan Hamid Karzai kuwakatama wahalifu na kupata udhibiti wa hali hiyo. Hivi sasa, biashara ya madawa ya kulevywa nchini Afghanistan ina thamani ya Euro bilioni 2.1 na inafanya theluthi ya uchumi wa nchi hiyo.madawa mengi ya kulevywa yanapatikana upande wa kusini mwa nchi hiyo katika jimbo la Helmand, ambalo hivi sasa linakabiliwa na ongezeko la mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wanaoungwa mkono na Taliban.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW