1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA : Repoti yaivuwa Sudan na mauaji ya halaiki

1 Februari 2005

Tume ilioachaguliwa na Umoja wa Mataifa imeishutumu serikali ya Sudan hapo jana kwa ukiukaji mkubwa wa makusudi wa haki za binaadamu huko Dafur lakini haikufikia hatua ya kuyaita machafuko ya umwagaji damu katika jimbo hilo kuwa sawa na mauaji ya halaiki.

Repoti hiyo inasema kipengee muhimu cha kuwepo nia ya kufanya mauaji ya halaiki inaonekana hakipo na imependekeza ukiukaji huo wa haki za binaadamu unafaa kushughulikiwa na Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake huko The Hague nchini Uholanzi hatua ambayo inapingwa na Marekani.

Repoti hiyo hususan inalaumu wanajeshi wa serikali na wanamgambo kwa kufanya mashambulizi ya kiholela ikiwa ni pamoja na kuuwa raia,kutesa,kuwalazimisha kutoweka,kuteketeza vijiji,ubakaji,uporaji na utekaji nyara pamoja na kuwapotezea watu makaazi katika eneo lote la jimbo la Dafur nchini Sudan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW