UN: Mtu 1 kati ya wanne duniani hana maji salama ya kunywa
26 Agosti 2025
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa zaidi ya watu bilioni mbili duniani kote bado wanakabiliwa na ukosefu wa upatikanaji wa maji ya kunywa yaliyo salama.UN imesema mtu mmoja kati ya wanne duniani hawakuweza kupata maji salamaya kunywa mwaka uliopita, huku zaidi ya watu milioni 100 wakiendelea kutegemea kunywa maji kutoka kwa vyanzo kama mito, mabwawa na mifereji. Nchi 28 ambako mtu mmoja kati ya wanne bado hana huduma za msingi za maji zipo barani Afrika.
Utafiti wa pamoja wa WHO na UNICEF unaonyesha kuwa dunia iko mbali sana na kufanikisha lengo la kufikia huduma hizi kwa wote ifikapo mwaka 2030. Gaza yakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji safiMkuu wa mazingira wa WHO, Ruediger Krech, amesema: "Maji na usafi wa mazingira si anasa: ni haki za kimsingi za binadamu, na hatua lazima ziharakishwe, hususan kwa jamii zilizotengwa zaidi.”
Ripoti hiyo ilichunguza viwango vitano vya huduma za maji ya kunywa. Kiwango cha juu, ambacho ni maji salama, kinamaanisha maji ya kunywa yanayopatikana nyumbani, yanayopatikana wakati wowote yanapohitajika na hayana uchafu wa kinyesi au kemikali.
Viwango vingine vinne ni: msingi yaani (huduma za maji zilizoboreshwa yanayohitaji chini ya dakika 30 kufikiwa), uchache ambayo nim aji (yaliyoboreshwa lakini yanayochukua muda mrefu zaidi kufikiwa), yasiyoboreshwa (kwa mfano maji kutoka kisima au chemchemi isiyo na kinga), na maji yaliyo ardhini kama vile mito, maziwa, bahari na ardhi oevu.
Ripoti hiyo imesema tangu mwaka 2015, watu milioni 961 wamepata maji ya kunywa yaliyosalama, huku kiwango cha upatikanaji kikipanda kutoka asilimia 68 hadi asilimia 74.
Idadi ya nchi zilizo ondoa kabisa matumizi ya maji yaliyo ardhini kwa kunywa imeongezeka kutoka 142 mwaka 2015 hadi 154 mwaka 2024, kulingana na utafiti huo.
"Usawa huu unawaathiri sana wasichana, ambao mara nyingi hubeba jukumu la kukusanya maji na hukumbana na changamoto zaidi wakati wa hedhi. Watoto wanapokosa maji salama, Mito ulimwenguni ilikauka zaidi mwaka 2023, katika kipindi cha miongo mitatu usafi na huduma za usafi wa mazingira, afya zao, elimu na mustakabali wao huwekwa hatarini,” alionya Cecilia Scharp, mkurugenzi wa UNICEF anayesimamia kitengo cha usafi wa mazingira. Wataalamu wanasema kuwa kwa sasa ahadi ya maji salamana usafi wa mazingira kwa kila mtoto inazidi kukosa kitimizika.
Kuhusu usafi wa mazingira, utafiti ulibaini kuwa watu bilioni 1.2 wamepata huduma za usafi wa mazingira zilizodhibitiwa kwa usalama tangu mwaka 2015, huku kiwango kikipanda kutoka asilimia 48 hadi asilimia 58.UN: Uhaba wa maji watishia mzozo wa kimataifa Hii imefanikishwa na vyoo vilivyoboreshwa ambavyo havishirikishwi na kaya nyingine, na ambapo kinyesi kinatupwa kwa usalama hapo hapo au kuondolewa na kutibiwa nje ya eneo.