1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu hali nchini Kosovo

24 Oktoba 2023

Misuguano kati ya serikali za mjini Pristina na Belgrade imekuwa mikali tangu afisa wa polisi alipouwawa mwezi uliopita kwenye uvamizi eneo la kaskazini la Kosovo.

Misuguano kati ya serikali za mjini Pristina na Belgrade imekuwa mikali
Misuguano kati ya serikali za mjini Pristina na Belgrade imekuwa mikali Picha: Vudi Xhymshiti/VX Photo/picture alliance

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake juu ya mazingira ya kutiliana shaka nchini Kosovo, ukitoa wito wa hatua muhimu za kutuliza hali ya mambo kati yake na Serbia.

Misuguano kati ya serikali za mjini Pristina na Belgrade imekuwa mikali tangu afisa wa polisi alipouwawa mwezi uliopita kwenye uvamizi eneo la kaskazini la Kosovo, kukiwa na madai aliuliwa na kikosi cha jeshi kilichowajumuisha Waserbia wa Kosovo.

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kosovo, Caroline Ziadeh, ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba tukio hilo la Septemba 24 lilichochea hali mbaya ya usalama ambayo tayari ilikuwa imevurugika na hali ya kushukiana ikiathiri asilimia kubwa ya wakazi hususan wa kaskazini mwa Kosovo na miongoni mwa jamii za Wakosovo wenye asili ya Serbia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW