UN yaanza uchunguzi dhidi ya ukiukaji wa haki Sudan
18 Januari 2024Mpango huo ulio na wanachama watatu umeanza kazi yake ya kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika mapigano hayo.
Kikosi hicho kimetoa wito kwa pande mbili zinazozozana katika mzozo huo kusimama na majukumu yao ya kuwalinda raia na kuhakikisha kwamba wachochezi wa matukio mabaya ya uhalifu wanachukuliwa hatua.
Sudan yasitisha mahusiano na IGAD kufuatia mwaliko wa Daglo
Wanachama wa kikosi hicho huru cha Umoja wa Mataifa waliteuliwa mnamo Desemba 18.
Mwenyekiti wa mpango huo ni Mohamed Chande Othman, ambaye ni jaji mkuu wa zamani wa Tanzania na atakuwa anashirikiana na Joy Ezeilo mkuu wa kitengo cha sheria katika chuo kikuu cha Nigeria na Mona Rishmawi aliye na uraia wa Jordan na Uswisi ambaye ni mtaalam huru wa zamani wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya haki za binadamu Somalia.