1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wabaini shughuli za M23 mashariki mwa DRC

6 Januari 2023

Wataalamu wa masuala ya kijasusi wa Umoja wa Mataifa wamesema wamebaini operesheni zinazoshukiwa kuwa za waasi wa M23 kwenye maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

DR Kongo Ein M23-Rebellen
Picha: GLODY MURHABAZI/AFP via Getty Images

Nyaraka za ndani za Umoja huo zilionesha jana kuwa M23 wamedhibiti maeneo mengine, wakati ambapo walitakiwa kuondoka huko.

Kitengo cha Ujasusi cha Umoja wa Mataifa kimesema katika ripoti yake ya siri kwamba waasi hao hawajaondoka kabisa katika jimbo la Kivu Kaskazini na mji wa Kibumba.

Ripoti hiyo imeleeza kuwa mapigano kadhaa yanayowahusisha M23 yameripotiwa wiki hii na kusababisha waasi hao kudhibiti maeneo zaidi ikiwemo Kitchanga na Nyamilima na kusababisha wasiwasi kwa raia.

M23 walipaswa kuondoka pia kwenye mji wa kimkakati wa Rumangabo hadi kufikia jana, lakini siku ya Jumatano Kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki kiliahirisha hafla iliyopangwa ya makabidhiano, kikisema bado kinatathmini hali ya usalama. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW