Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi juu ya Burkina Faso
10 Februari 2022Hata hivyo baraza hilo halikulitaja tukio hilo kama mapinduzi ya kijeshi ama hata kulilaani kwa uwazi.
Kulingana na toleo la awali la waraka ambao shirika la habari la AFP liliupata, baraza hilo limeutolea mwito utawala wa kijeshi kuratibu mara moja kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba nchini humo, lakini ombi hilo liliondolewa na Urusi, hii ikiwa ni kulingana na mwanadiplomasia ambaye hakutaka kutambulishwa.
soma zaidi: ECOWAS kutoiwekea vikwazo Burkina Faso
Kwenye azimio ambalo lilipitishwa na wanachama 15 wa baraza hilo aidha limeomba kuachiwa huru kwa rais Marc Christian Kabore pamoja na maafisa wengine wa serikali, lakini pia kupewa ulinzi.
Aidha, limeeleza kuunga mkono juhudi za upatanishi za kikanda ili kusuluhisha mzozo uliopo, baada ya kufunguliwa kwa ofisi ya pamoja ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa nchini humo.