1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

UN yafanya mazungumzo na Urusi kuhusu usafirishaji nafaka

10 Oktoba 2023

Mkuu wa Shirika la UNCTAD Rebeca Grynspan, amekutana na maafisa wa Urusi mjini Moscow kwa mazungumzo yenye lengo la kuwezesha ufikiaji bila vizuizi wa nafaka na mbolea kutoka Ukraine na Urusi katika masoko ya kimataifa

Mkuu wa Shirika la UNCTAD Rebeca Grynspan
Mkuu wa Shirika la UNCTAD Rebeca GrynspanPicha: www.segib.org

Dujarric amesema kuwa mkuu wa uratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja huo wa Mataifa Martin Griffiths pia alihudhuria mkutano huo kwa njia ya video. Dujarric ameongeza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anaendeleza jitihada zake za kuwezesha ufikiaji usio na vizuizi wa masoko ya kimataifa kwa bidhaa za chakula na mbolea kutoka Ukraine na Urusi.

Soma pia:Urusi imejiondoa katika mkataba wa nafaka

Dujarric amesema mashauriano kati ya wakuu hao wawili Grynspan na Griffiths pamoja na Urusi, yanafanyika kwa kuzingatia lengo hilo.Umoja wa Mataifa umelaumu vita vya Urusi nchini Ukraine kwa kuzidisha mzozo wa chakula duniani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW