1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wahofia kutofanyika uchaguzi nchini Haiti

23 Oktoba 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewaonya viongozi wa Haiti kuwa muda wa kurejesha usalama na kuandaa uchaguzi mkuu nchini humo unasonga.

Viongozi wa Haiti Vladimir Paraison Laurent Saint-Cyr wakipeana mikono
Viongozi wa Haiti Vladimir Paraison Laurent Saint-Cyr wakipeana mikonoPicha: Fildor Pq Egeder/REUTERS

Onyo hilo la Umoja wa Mataifa linakuja huku muda wa mwisho wa kubuniwa kwa serikali mpya ukiwa unakaribia.

Haiti bado haijatangaza tarehe ya uchaguzi mkuu ambao utakuwa wa kwanza katika kipindi cha karibu mwongo mmoja, wakati ambapo uhalifu unaofanywa na magenge ukiwa unazidi kuuzonga mji mkuu na viunga vyake.

Maandalizi ya kiufundi ya uchaguzi huo lakini yameshaanza. Baraza la muda la uchaguzi nchini Haiti limesema kuwa awamu ya kwanza ya uchaguzi huo itagharimu karibu dola milioni 140.

Wizara ya sheria ya haiti imetangaza kuwa zaidi ya vyama 220 vya kisiasa vimeanza mchakato wa kujisajili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW