Umoja wa Mataifa wakisia ukuaji duni wa uchumi wa dunia 2024
5 Januari 2024Umoja wa Mataifa jana Alhamisi umechapisha utabiri wa ukuaji wa uchumi ulimwenguni kwa mwaka 2024, ulioonyesha utakabiliwa na changamoto zinazoanzia kwenye migogoro inayoongezeka, biashara iliyodhoofu ya kimataifa, viwango vya juu vya riba na kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa.
Kwenye ripoti hiyo, Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa ukuaji wa uchumi kimataifa utapungua hadi asilimia 2.4 mwaka huu kutoka wastani wa asilimia 2.7 ya mwaka 2023.
Soma pia: Watafiti: Uchumi unaimarika lakini lipo ombwe kwa Wamarekani
Hata hivyo makisio hayo bado yako chini ya kiwango cha ukuaji cha asilimia 3.0 cha kabla ya mlipuko wa janga la UVIKO -19 mnamo mwaka 2020, imesema ripoti hiyo.
Utabiri huu wa Umoja wa Mataifa uko chini kuliko wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF wa mwezi Oktoba na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OEC uliochapishwa mwishoni mwa Novemba mwaka uliopita.