1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

UN yahofia ukiukaji wa haki unaofanywa na Urusi, Ukraine

28 Aprili 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo zna hofu kuhusiana na suala la ukiukaji wa haki za binaadamu unaofanywa na majeshi ya Urusi na kampuni za kibinafsi za kijeshi nchini Ukraine.

UN Generalsekretär Antonio Guterres / New York
Picha: Fatih Aktas/AA/picture alliance

Kamati ya Umoja huo inayohusiana na kuangamizwa kwa ubaguzi wa rangi katika utafiti wake kuhusu Urusi imesema kumekuwa na vitendo vya watu kupotezwa, mateso, ubakaji na mauaji ya kiholela.

Ubalozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa haujatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hiyo. Umoja wa Mataifa unasema Urusi, ambayo imekataa kutoa taarifa kuhusiana na vita hivyo, imekuwa ikikanusha kufanya uhaini na kuwashambulia raia wa Ukraine makusudi.

Soma zaidi: UN: Vita vya Ukraine vimesababisha ukiukwaji wa haki

Urusi pia imekanusha kuwapeleka kwa nguvu watoto wa Ukraine nchini Urusi ikisema imewaokoa tu na kuwapeleka mahali salama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW