1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wahofia uvunjwaji haki za binaadamu Uganda

27 Julai 2023

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanahofia kwamba kumekuwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa nan vyombo vya dola nchini Uganda katika miaka ya hivi karibuni.

Yoweri Musevini to sign anti-LGBT law
Picha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Katika ripoti yake iliyoitowa jana, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binaadamu imesema kumekuwa kukishuhudiwa kamatakamata inayowalenga wapinzani wa kisiasa, waandishi wa habari, mawakili, watetezi wa haki za binadamu, makahaba na wapenzi wa jinsia moja.

Soma zaidi: Biden akosoa sheria ya Uganda dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuhimiza kufutwa

Kamati hiyo imezitaka mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuifutilia mbali sheria inayopendekeza adhabu ya kifo kwa baadhi ya vitendo vinavyofanywa na wapenzi wa jinsia moja.

Ripoti hiyo ni ya kwanza ya Umoja wa Mataifa kuhakiki mambo yalivyo nchini Uganda tangu mwaka 2004.

Msemaji wa serikali ya Uganda hakupatikana kutoa tamko kuhusiana na ripoti hiyo.