1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaidhinisha kikosi cha kupambana na uhalifu Haiti

1 Oktoba 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne limepiga kura kuidhinisha kikosi cha kimataifa kwa ajili ya kupambana na magenge ya uhalifu nchini Haiti.

Port-au-Prince, Haiti  2025 | Polisi wa Kenya wakifanya doria kwenye kitongoji cha Delmas
Kikosi kipya kinatarajiwa kuwa na takribani askari 5,500Picha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Kikosi kipya kitakachokuwa na askari wapatao 5,500, kinatarajiwa kuchukua nafasi ya Kikosi cha Usalama cha Kimataifa, MSS kilichopo sasa kinachoongozwa na Kenya, ambacho mamlaka yake inamalizika tarehe 2 Oktoba.

Marekani na Panama ziliwasilisha rasimu ya azimio la kuanzishwa kwa kikosi hicho.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz ameipongeza hatua hiyo.

''Kikosi kipya kitakuwa na uwezo wa kuwaajiri hadi askari 5,000, kwa sababu ya msaada wa vifaa kutoka ofisi ya misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti," alifafanua Waltz.

Marekani yaupongeza Umoja wa Mataifa

Waltz amesema wanalipongeza Baraza la Usalama kwa kuchukua hatua hiyo na kuonyesha kuwa Umoja wa Mataifa bado una uwezo wa kutimiza lengo lake kuu la kudumisha amani na usalama wa kimataifa.

Nchi 12 wanachama kati ya 15 walipiga kura kuunga mkono azimio hilo, huku China, Urusi na Pakistan zikijizuia kupiga kura.

Ubalozi wa Marekani nchini Haiti umesema ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uko wazi, kwamba enzi ya kutochukuliwa hatua kwa wote wanaotaka kuvuruga amani nchini humo, zimekwisha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW