Umoja wa Mataifa waionya Libya kutumbukia kwenye mgawanyiko
16 Februari 2024Bathily aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kuna dalili nyingi za kutisha za kutokea kwa mgawanyiko huo na aliwataka viongozi wote wa kisiasa kuweka kando "maslahi yao binafsi" na kukaa kitako kufanya mazungumzo na kufikia maelewano kudumisha hadhi ya nchi hiyo.
Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu machafuko Libya
Bathily aliongeza kuwa kusita kufanya hivyo kunatilia mashaka sio tu kujitolea kwao katika uchaguzi, lakini pia kwa umoja na mustakabali wa nchi hiyo.
Bathily aliliambia Baraza hilo kuwa katika mazungumzo yake ya hivi karibuni na wadau wakuu, hakuna aliyebatilisha msimamo wa awali na kila mmoja ameweka masharti ya kushiriki katika mazungumzo ya kutatua masuala yanayozozaniwa, ambayo huenda yakafungua njia kwa uchaguzi unaosubiriwa kwa muda mrefu.