Umoja wa Mataifa wakusanya dola bilioni 1.2 kuisaidia Yemen
28 Februari 2023Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa misaada ya Kiutu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, alisema fedha hizo zitasaidia pakubwa kupeleka misaada mwaka huu nchini Yemen, kwa mamilioni ya raia huko wanaokabiliwa na njaa, wakati huu kukiwa na matumaini kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano, huenda yakafungua nafasi ya kupatikana amani ya kudumu.
Umoja wa Mataifa wafadhaishwa na kukosekana fedha za kuisaidia Yemen
Katika Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva, kiwango cha fedha kilichotolewa cha dola bilioni 1.2 sio kile kilichotarajiwa cha dola bilioni 4.3, lakini Umoja wa Mataifa umesema huenda dola bilioni 2 zikapatikana mwishoni mwa wiki hii katika mkutano huo wa wahisani, wa kuhamasisha utoaji wa msaada kwaajili ya Yemen.
Huu ni mkutano wa saba wa kuisaidia Yemen unaofanyika kila mwaka kwa mwaka wa saba sasa. Umoja wa Mataifa unatumai mkutano ujao utajikita katika kuijenga upya Yemen kuliko kuzungumzia namna raia wa taifa hilo wanavyokufa kwa njaa.
Umoja wa Mataifa watarajia kukusanya dola bilioni 4.27 kwa ajili ya Yemen
Katika Mkutano huo Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema Uchumi wa Yemen pamoja na taasisi zake vimesambaratishwa vibaya kutokana na mgogoro uliopo huku akiahidi msaada wa dolla milioni 444.
Msaada uliotolewa ni wa kibaguzi
Huku hayo yakiarifiwa Umoja huo unakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 21.7 nchini Yemen wanahitaji msaada wa kiutu.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Msaada wa Kiutu la Norwegian Refugee Council Erin Hutchinson, amesema dunia imeitelekeza Yemen wakati huu mgumu kwa kutoa robo tu ya kiwango kilichohitajika. Amesema kilichofanyika kinaonesha wazi kwamba baadhi ya watu wanathaminiwa kuliko wengine.
Saudi Arabia na Wahouthi watafuta suluhu Yemen
Hata hivyo Mataifa mengi yalitaka kusitishwa kwa kanuni iliyowekwa na waasi wa Houthi inayowalazimisha wanawake wakiwemo wafanyakazi wa kike wa kutoa misaada kuandamana na walezi wa kiume jambo linalotatiza shughuli za kutoa msaada. Kwa upande wake waziri Mkuu wa Yemen Maeen Abdulmalek Saeed amesema kumaliza janga la kibinaadamu nchini humo kutaanza pale tu vita vitakapokwisha kikamilifu nchini humo.
Yemen imekumbwa na mapigano makali kuanzia mwaka 2014 kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na serikali inayotambulika kimataifa inayoungwa mkono na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
Mamilioni ya watoto,wanawake hatarini Yemen
Tangu wakati huo vita hivyo vimesababisha maelfu ya vifo na kulifanya taifa hilo kukabiliwa na tatizo kubwa la njaa. Makubaliano ya kusitisha mapigano yalioanza mwezi Aprili mwaka jana yalimalizika mwezi Oktoba, lakini baadhi ya maeneo yamekuwa na utulivu mdogo.
Chanzo: afp