Janga
Misaada ya kuwasaidia Walibya walionusurika yakusanywa
13 Septemba 2023![Libyen | Überschwemmung und Hochwasser in Libyen](https://static.dw.com/image/66797755_800.webp)
Matangazo
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa,Stephan Dujarric, amefahamisha kwamba taasisi hiyo inashirikiana na watu ndani ya Libya na washirika wake wa kimataifa kupata msaada wa dharura wa kibinadamu utakaopelekwa katika maeneo yaliyoathirika nchini humo.
Amesema timu ya Umoja wa Mataifa iko nchini Libya na inashirikiana na maafisa wa ndani kusaidia kutathmini juhudi za kutowa msaada na mahitaji.
Kimbunga Daniel chaua watu zaidi ya 2,000 Libya
Kwa mujibu wa shirikisho la kimataifa la shirika la msalaba mwekundu na hilali nyekundu, Waokoaji bado wanaendelea na operesheni za kutafuta manusura huku ikiripotiwa kwamba watu 10,000 bado hawajulikani waliko kufuatia kimbunga Daniel.