1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa walaani unyanyasaji Myanmar

24 Agosti 2023

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani unyanyasaji uliopitiliza na mauaji ya raia Myanmar. Wameutaka utawala wa kijeshi kusitisha mashambulizi, kumuachia huru Aung San Suu Kyi, na kuheshimu haki.

New York | Eine Sitzung des Sicherheitsrats der Vereinten Nationen
Picha: ED JONES/AFP/Getty Images

Wanachama 13 kati ya 15 wameunga mkono taarifa ya pamoja inayosema hakukua na hatua za maana za utekelezaji wa azimio la kwanza kabisa la baraza hilo kuhusu Myanmar lililopitishwa Disemba mwaka jana.

Urusi na China zenye mahusiano na utawala huo wa kijeshi hazikupiga kura, pamoja na India ambayo muhula wake wa miaka miwili kwenye baraza hilo umekamilika.

Azimio hilo aidha, limetoa mwito wa utekelezwaji kamili wa mpango wa wanachama 10 wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia wa Aprili 2021, uliokubaliwa na utawala wa kijeshi wa Myanmar, uliowataka kusitisha mapigano na mazungumzo ambao, utekelezwaji wake unasuasua.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW