1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Rais wa zamani wa Iraq awa mkuu mpya wa UNHCR

19 Desemba 2025

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Alhamisi lilimuidhinisha Rais wa zamani wa Iraq Barham Salih kuwa mkuu ajaye wa shirika la wakimbizi, UNHCR, akiwa ni kwanza kutoka Mashariki ya Kati tangu mwishoni mwa miaka ya 1970.

Irak | Rais Barham Salih
Rais wa zamani wa Iraq Barham Salih akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (haonekani) huko Baghdad, Iraq mnamo Septemba 2, 2020. Picha: Murtadha Al-Sudani/AA/picture alliance

Baraza hilo lenye wanachama 193 lilimchagua mwanasiasa huyo wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 65 kuwa kamishna mkuu wa UNHCR kwa makubaliano na Rais wa Baraza Kuu Annalena Baerbock.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amemsifu kiongozi huyo kutokana na uzoefu wake kwenye eneo la diplomasia, siasa na utawala na kumtaja kama mbunifu wa mageuzi ya kitaifa.

Salih anachukua nafasi ya Filippo Grandiambaye muda wake wa awamu ya pili unamalizika Disemba 31. Kipindi cha Salih kitaanza Januari Mosi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW