1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaVenezuela

Umoja wa Mataifa waomba mil. 296 za kuisaidia Venezuela

9 Julai 2026

Umoja wa Mataifa jana Jumatano ulitoa wito wa dharura wa karibu dola milioni 300 za misaada baada ya tetemeko la ardhi nchini Venezuela. Idadi ya waliofariki kutokana na janga hilo imepindukia watu 3,800.

Venezuela Caraballeda 2026 | Kazi ya usafi baada ya matetemeko ya ardhi ya Juni 24
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa dharura wa mamilioni ya dola kwa ajili ya kuisaidia Venezuela iliyokumbwa na matetemekoPicha: Raul Arboleda/AFP

Akizungumza katika mkutano kuhusu janga hilo, Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher, amesema wafadhili wameanza kujitokeza kufuatia ombi hilo baada ya ombi hilo la dola milioni 296 ili kutoa msaada wa haraka kwa watu milioni 1.3 katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Katika hatua nyingine, serikali ya Venezuela imetoa wito wa kuachiliwa kwa mali zilizozuiwa nje ya nchi ili kusaidia kupata fedha kwa ajili ya shughuli za uokozi na ujenzi upya wa taifa hilo.

Mali hizo ni pamoja na takriban tani 30 za dhahabu ya Venezuela zinazozuiliwa chini ya vikwazo vya Uingereza.

Mahitaji ya kibinadamu yameendelea kuwa makubwa kufuatia moja ya majanga makubwa zaidi ya tetemeko la ardhi huko Amerika ya Kusini, ambalo limewaacha maelfu ya watu bila makazi na wengine wengi wakiwa bado hawajulikani walipo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW