1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan

Burhan akutana na Salva Kiir kujadili mzozo wa Sudan

4 Septemba 2023

UNHCR yasema mahitaji ya wakimbizi wa vita Sudan yapindukia mara mbili zaidi ya ilivyokadiriwa. Shirika hilo na mengine yametoa mwito wa kupatiwa dola bilioni moja za kununua msaada wa mahitaji muhimu.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-BurhanPicha: Sudanese Army/AFP

Wakati Umoja wa Mataifa ukiomba dola bilioni 1 ili kuwasaidia raia wa Sudan wanaokimbia machafuko nchini humo, Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amefanya mazungumzo hii leo na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kujadili juu ya hali ya mzozo unaoendelea nchini mwake.

Soma zaidi: UN:Tunahitahi msaada mara mbili zaidi kwa wasudani

Jenerali Abdel-Fattah Burhan, Mkuu wa jeshi la Sudan ametua leo katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba  na kupokelewa na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. Viongozi hao wawili walikagua gwaride la heshima na kisha baadaye kufanya mazungumzo yaliyoangazia mzozo unaoendelea Sudan.

Safari ya pili nje ya nchi kwa Burhan

Hii ni safari ya pili ya Burhan nje ya nchi baada ya ile ya wiki jana aliyoifanya mjini Cairo tangu machafuko yalipozuka nchini Sudan katikati ya mwezi Aprili mwaka huu kati ya jeshi la serikali na kikosi cha msaada wa dharura  cha RSF kinachoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo.

Rais wa Sudan Kusin Salva Kiir MayarditPicha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Wakati mkutano huo ukiendelea, Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ali al-Sadiq ambaye aliongozana na Burhan kwenye mkutano huo ametumia mtandao wa kijamii wa Facebook wa Ofisi ya Rais Sudan kuunga mkono majadiliano hayo, aliandika, "Sisi Sudan tunaona kuwa Sudan Kusini ndio nchi bora zaidi ya kutafakari mzozo wa Sudan, kwa sababu tumekuwa nchi moja kwa muda mrefu na tunajuana, tunajua shida na tunajua mahitaji yetu." 

Soma zaidi:  Mkuu wa jeshi la Sudan arudi nyumbani baada ya ziara yake ya kwanza nje ya nchi

Sudan Kusini ambayo ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Sudan mwezi Julai 2011 baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe inajaribu kuchukua jukumu la upatanishi ili kumaliza mzozo huo kwa majirani wake wa upande wa kaskaziMkuu wa jeshi la Sudan arudi nyumbani baada ya ziara yake ya kwanza nje ya nchini.

Kambi ya wakimbizi wa Sudan nchini ChadPicha: Marie-Helena Laurent/WFP/AP/picture alliance

Kwa upande wa Sudan Kusini, Waziri anayeshughulikia masuala ya baraza la mawaziri nchini humo Martin Elia Lomuro ameeleza kwamba Rais Kiir ndiye mtu pekee ana uelewa na ujuzi kuhusu Sudan na kwamba anaweza kupata suluhu la mgogoro wa Sudan.

Umoja wa mataifa watoa wito wa msaada zaidi kwa wasudan

Siku ya Jumatatu, Umoja wa Mataifana mashirika mengine 64 ya kibinadamu yaliomba dola bilioni 1 ili kusaidia raia wa Sudan zaidi ya milioni 1.8 waliokimbia vita na kutafuta hidhahi katika nchi za Misri, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia na Sudan Kusini.

Shirika la kimataifa la uhamiaji UNHCR limesema kwamba fedha hizo ni ongezeko la mara mbili ya kile kilichokuwa kimekadiriwa mwezi mei mwaka huu na kwaba mahitaji yanaendelea kupanuka zaidi.

Kulingana na ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa, mapigano kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Burhan na lile la RSF linaloongozwa na Mohammed Hamadan Dagalo, zaidi ya watu 4000 wanakadiriwa kupoteza maisha ingawa wanaharakati na madaktari wanaeleza kwamba huenda idadi ni kubwa zaidi ya iliyorekodiwa.

      
      

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW