Umoja wa Mataifa waomba msaada zaidi wa kibinadamu Kongo
20 Aprili 2024Mratibu wa msaada wa kibinadamu wa Umoja huo nchini Kongo, Bruno Lemarquis, alisema jana kwamba kufikia mwezi Aprili, ni asilimia 15 tu ya fedha zinazohitajika kuwasaidia watu milioni 8.7 zilizokuwa zimepatikana na kwamba mahitaji ni makubwa zaidi kuliko wanachoweza kutoa.
Dola bilioni 2.6 za msaada zinahitajika kwa mwaka huu
Umoja wa Mataifa unahitaji angalau dola bilioni 2.6 kwa mwaka huu, lakini unahofia kuwa kuwepo kwa migogoro mingi duniani kumeufunika mgogoro huo wa Kongo.
Soma pia: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama Mashariki mwa Kongo
Mratibu huyo amesema kwa sasa wanalazimika kutoa msaada huo kwa kuzingatia vipaumbele, kutokana na kiwango kidogo cha ufadhili wa shughuli za kibinadamu nchini Kongo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.