1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonesha wasiwasi kuhusu hali nchini Guinea Bissau

27 Novemba 2025

Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi kuhusu hali ya Guinea Bissau baada ya jeshi kutangaza kufanya mapinduzi. Mapinduzi hayo yaliyotokea baada ya milio ya risasi kusikika karibu na ikulu Jumatano.

Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi kuhusu hali Guinea Bissau
Rais wa Guinea Bissau aliyepinduliwa Umaro Sissoco EmbaloPicha: Kristina Kormilitsyna/Sputnik/REUTERS

Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake kuhusu hali nchini Guinea Bissau baada ya jeshi kupitia Televisheni ya taifa kutangaza kuchukuwa udhibiti kamili wa taifa hilo. Kupitia msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres amezitaka pande zote kufuata na kuheshimu utawala wa sheria na kuahidi kufuatilia hali nchini humo.

Milio ya risasi kabla ya jeshi kutangaza mapinduzi

Jumatano, Milio ya risasi ilisikika karibu na Ikulu ya Rais Umaro Sissoco Embalo, nchini humo siku tatu baada ya uchaguzi wa rais na wabunge. Kwenye uchaguzi huo Embalo, na mgombea wa upinzani walijitangazia ushindi.

Rais Embalo aliyetarajiwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo ameviambia vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa ameondolewa mamlakani na kukamatwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW