1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waongeza makampuni 68 kwenye orodha nyeusi

26 Septemba 2025

UN yaongeza takriban makampuni 70 zaidi kwenye orodha nyeusi ya makampuni kutoka nchi 11 inayodai yanashiriki kukiuka haki za binadamu za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi kupitia uhusiano wa kibiashara.

Nembo ya Airbnb, moja ya makampuni yalioorodheshwa na UN kwenye orodha nyeusi
Nembo ya AirbnbPicha: Da Qing/HPIC/dpa/picture alliance

Orodha hiyo mpya inaanganzia makampuni yanayofanya biashara zinazodhaniwa kuunga mkono makazi hayo yanayozingatiwa na wengi kuwa kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Hii inajumuisha makampuni kadhaa kama ya wauzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na

watoa huduma za usalama, usafiri na kifedha.

Miongoni mwa makampuni yalioorodheshwa ni  kundi la makampuni la Expedia lenye makao yake Marekani, Booking Holdings Inc. na Airbnb, Inc.

Nchi za makampuni yalioko kwenye orodha nyeusi

Orodha hiyo, inayojulikana rasmi kama "kanzidata ya makampuni," sasa ina makampuni 158, idadi kubwa kutoka Israel. Mengine ni kutoka Marekani, Canada, China, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania, Ureno, Uholanzi na Luxemburg.

Wakati Makampuni mpya 68 yameongezwa kwenye orodha hiyo leo Ijumaa, saba yameondolewa.

Katika awamu hii, idadi jumla ya makampuni 215 ya biashara yalifanyiwa tathmini  lakini mamia zaidi yataangaziwa katika siku zijazo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW