1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waongeza muda wa kikosi cha polisi Haiti

1 Oktoba 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja hatua ya kurefusha muda wa kubakia nchini Haiti kwa mwaka mmoja zaidi kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya kukabiliana na magenge ya kihalifu.

Kenya, Haiti, Umoja wa Mataifa
Rais William Ruto wa Kenya akiwaaga maafisa wa jeshi la polisi waliokwenda kuhudumu nchini Haiti.Picha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Baraza hilo la usalama kuukataa mwito uliotolewa na Haiti wa kuanzisha mazungumzo ya kukibadilisha kikosi hicho kuwa ujumbe wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa.

Soma zaidi: Marekani yaachana na wazo la jeshi la UM Haiti

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, alisema uamuzi uliopitishwa kwa kauli moja na wanachama 15 wa Baraza la Usalama unatuma ujumbe mzito kwa Haiti.

Balozi huyo alisema hatua hiyo ni juhudi za kusaidia kurudisha usalama na uthabiti katika taifa hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW