JamiiHaiti
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali mbaya inayoendelea Haiti
23 Aprili 2024Matangazo
UNICEF imesema vurugu hizo zinayaweka hatarini maisha ya watoto wapatao 58,000 ambao wanakabiliwa na viwango vya juu vya utapiamlo.
Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema theluthi mbili ya watoto wa Haiti wanahitaji misaada, huku wanawake na wasichana wakilengwa na "viwango vilivyokithiri" vya unyanyasaji wa kijinsia na kingono.
Russell ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali nchini Haiti ni mbaya mno na inazidi kuwa mbaya kila siku, hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince unaodhibitiwa kwa asilimia 90 na magenge hayo, sasa unakaribia kuzingirwa kabisa kutokana na vizuizi vya angani, baharini na nchi kavu.