1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Umoja wa Mataifa waonya kuongezeka kwa wakimbizi wa Sudan

16 Oktoba 2024

Idadi ya wakimbizi inazidi kuongezeka ambapo watu 25,000 wamekimbilia nchi jirani ya Chad katika wiki ya kwanza ya mwezi huu wa Oktoba.

Umoja wa Mataifa waonya kuongezeka kwa wakimbizi wa Sudan
Umoja wa Mataifa waonya kuongezeka kwa wakimbizi wa SudanPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan anayehusika na masuala ya wakimbizi Mamadou Dian Balde, amesema idadi hiyo ya watu milioni tatu huenda ikaongezeka maradufu ndani ya wiki mbili hadi tatu zijazo, na kusisitiza kuwa janga hilo linalohusishwa moja kwa moja na kuongezeka kwa ukatili katika mzozo huo.

Vita hivyo vilivyoanza mwezi Aprili mwaka 2023 kati ya jeshi la Sudan likiongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na vikosi vya Msaada wa Haraka vya RSF vinavyoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW