Umoja wa Mataifa waonya utatuzi mkwako wa Libya
27 Julai 2023Hii ni baada ya mabunge mawili pinzani kupendekeza kuundwa kwa serikali mpya ya mpito, kama hatua ya mwanzo ya kuelekea kwenye uchaguzi.
Mpango huo wa Umoja wa Mataifa katika taarifa umesema, hatua za upande mmoja kama ilivyojaribiwa awali, zinaweza kuwa na athari mbaya kwa Libya na kusababisha msukosuko zaidi na machafuko.
Soma: Walinzi wa pwani ya Libya wawaokoa wahamiaji wa Kiafrika katika msitu karibu na Tunisia
Pande hizo mbili, Baraza la wawakilishi lililoko mashariki mwa nchi hiyo na Baraza Kuu la Taifa lililoko Libya, ziliunga mkono pande tofauti wakati wa mapigano kati ya mirengo ya mashariki na magharibi, ambayo tangu mwaka 2020 yametulia.
Umoja wa Mataifa unataka njia ya wazi kuelekea kufanyika uchaguzi kama sehemu ya suluhisho la kudumu kwa mzozo uliodumu kwa miaka 12 wa Libya.